Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, swala ya jamaa ni miongoni mwa ibada ambazo, pamoja na thawabu binafsi, zina faida na baraka nyingi za kijamii, kuhakikisha masharti na usahihi wa swala hiyo ni jambo la muhimu sana, miongoni mwa masharti hayo ni “kuungana safu”, yaani maamum wanapaswa kuungana na imamu au na safu za mbele bila ya kipingamizi au umbali usio wa kawaida.
Hata hivyo, wakati mwingine kutokana na wingi wa watu au namna ya kusimama kwa wanawake, muungano wa moja kwa moja kwa baadhi ya wanaume hauwezekani, hapo huibuka swali: Je, inajuzu wanaume hao kuunganishwa na jamaa kupitia safu ya wanawake? Mtukufu Ayatullah Khamenei amejibu istiftaa hii kama ifuatavyo:
Swali:
Ikiwa katika swala ya jamaa wanawake watasimama kwa namna ambayo baadhi ya wanaume hawawezi kuungana moja kwa moja na safu ya wanaume, je inasihi wanaume hao kuungana kupitia upande au nyuma ya wanawake na kwa kupitia wanawake hao waungane na jamaa?
Jawabu:
Kuungana safu ya wanaume kwa kupitia wanawake kutakuwa sahihi kwa masharti mawili:
Mosi, Ikiwa mwanamke na mwanaume watakuwa wameambatana au mwanamke kama atakuwa mbele, basi lazima pawepo angalau na umbali kiasi baina yao, hata kama ni maharim.
Pili, Pasiwepo pazia au kizuizi kingine baina ya wanawake na wanaume (iwe kabla au baada ya safu ya wanawake), vinginevyo, kwa mujibu wa ihtiyat ya wajibu, swala ya jamaa ya wanaume inayounganishwa kupitia wanawake haitakuwa sahihi.
Maoni yako